Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Utaratibu wa Kizayuni (Israel) katika mazungumzo ya kusitisha mapigano umeleta pendekezo linalolenga kuvamia takribani asilimia 40 ya Ukanda wa Gaza, likiwemo jiji lote la Rafah.
Kwa mujibu wa mpango huo, majeshi ya Israel yatabaki katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa mji wa Gaza, Rafah, Beit Lahia, Beit Hanoun, Khuza’a, na maeneo ya mpakani yenye upana wa hadi kilomita 3 ndani ya ardhi ya Gaza.
Katika eneo la Rafah, mpangilio wa wakimbizi umefanywa kwa namna ambayo utarahisisha uhamisho wa kulazimishwa wa wananchi.
Kwa mujibu wa mpango huo, asilimia 40 ya Gaza itabaki chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa utawala wa Kizayuni, na Wapalestina zaidi ya 700,000 watanyimwa haki ya kurejea katika nyumba zao.
Zaidi ya hayo, utawala wa Kizayuni unataka kuanzisha eneo la mpaka la usalama na kambi za muda, ambazo baadaye zitabadilishwa kuwa vituo vya kifungo na uhamisho wa kulazimishwa.
Your Comment